Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2017

Tundu Lissu afunguka

Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu ambaye anaendelea na matibabu nchini Kenya jijini Nairobi amefunguka na kusema kuwa wanaendelea kupigana na watashinda vita hiyo. Lissu amesema hayo baada ya kukutana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jusa Ladhu alipomtembelea jijini Nairobi katika hospitali anayopatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma. "Leo nina furaha sana kwa kupata fursa ya kumtembelea sahib na ndugu yangu, Tundu Lissu, Nairobi Hospital anakoendelea kupata matibabu baada ya kupigwa risasi zipatazo 16 mwilini Septemba 7, mwaka huu. Amenambia nikufikishieni ujumbe huu: "We keep up the fight and we shall win" alindika Jussa kwenye mtandao wake wa twitter Mbali na hilo Jussa amedai kuwa afya ya Tundu Lissu kwa sasa inaendelea vizuri sana "Anaendelea vizuri sana. Mimi leo nilivyomuona sikuamini jinsi anavyopata nafuu. Kwa hakika ni Qudra ya Mwenyezi Mun

Jeshi la Malaysia lipo tayari kuukomboa mji wa Jerusalem

Hishammuddin Tun Huseyin, Waziri wa ulinzi wa Malaysaia asema kuwa jeshi la lake lipo tayari wakati wowote kusaidia mji mtakatifu wa Jerusalem. Taarifa zilizotolewa na jarida la Bernama nchini Malaysia limesema kuwa waziri wa ulinzizi Hishammuddin Tun Hüseyin aliyazungumza hayo katika mkutano wa chama  baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuwa serikali yake inatambua jiji la Jerusalem kama mji mkuu wa Israel. Waziri wa ullinzi wa Malaysia amenukiliwa akisema kuwa  ni wajibu kuwa tayari kwa hali yeyote  na tunasubiri uongozi ili kuukomboa mji wa Jerusalem. Vile vile waziri wa huyo wa ulinzi amesema kuwa mzozo uliopo tuombe ili usiweze  kugeuka na kuwa  janga kubwa.

Marekani: Wayahudi waandamana kupinga uamuzi wa Trump kuhusu Jerusalem

Wayahudi wanaopinga  mfumo wa kizayuni wameandamano mjini New York  kupinga uamuzi wa rais wa Marekani kutangaza kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel. Wayahudi hao wanaotambulika kwa jina la Neturei Karta walikuwa na mabango mbele ya  makao makuu ya Umoja wa Mataifa  wakikemea uamuzi wa Trump kuhusu jiji la Jerusalem. Wayahui hao wanaituhumu serikali ya Israel kuupora mji mtakatifu.

MAGAZETI YA LEO 10/12/2017

BABU SEYA, PAPII KOCHA HAWA HAPA WAACHIWA KUTOKA GEREZANI

Mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ wametoka katika gereza la Ukonga jioni hii baada ya kusota kwa miaka 13. Wanamuziki hao ‘baba na mwana’ walitoka katika kifungo cha maisha baada ya kupata msamaha wa Rais John Magufuli leo Jumamosi Desemba 9, mwaka 2017. JPM alitoa msamaha kwa baadhi ya wafungwa alipokuwa akihutubia Taifa kusherehea miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miongoni mwa waliopata ahueni hiyo ni Babu Seya na Papii Kocha. “Babu, babu, babu,” zilikuwa ni kelele za mashabiki na ndugu zake waliompokea Babu Seya na Papii Kocha waliokuwa wametoka gerezani wakiwa na magitaa yao mgongoni. Babu Seya aliyeonekana mtanashati alionekana anapunga mkono wa kulia kama mtu asiyeamini huku Papii Kocha akipunga mkono akionekana kufurahia na kuzungumza na mashabiki. Walisindikizwa na askari magereza mpaka nje na kulikuwa na foleni kubwa kutokana na tukio hilo.

Zanzibar Heroes yafuzu

Timu ya taifa ya kandanda ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya fainali ya CECAFA Senior Challenge baada ya kutoka suluhu na Kenya jioni hii. Mchezo huo umemalizika jioni hii kwenye uwanja wa Kenyatta uliopo County ya Machakos ambapo Zanzibar Heroes imeilazimisha suluhu ya 0-0 timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars. Zanzibar Heroes imefuzu hatua hiyo baada ya kushinda michezo miwili dhidi ya Rwanda na Kilimanjaro Stars na kutoka sare moja ya leo dhidi ya Kenya, hivyo kuongoza kundi A. Zanzibar Heroes sasa imefikisha alama 7 na kufuzu hatua hiyo ikifuatiwa na Kenya yenye alama 5 ambayo itasubiri matokeo yake ya mchezo wa mwisho dhidi ya Kilimanjaro Stars. Mapema mchana leo timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imetolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa mabao 2-1 na timu ya taifa ya Rwanda.

Mtoto wa Babu Seya, Michael Nguza afunguka haya baada ya familia yao kuwa huru

Dar es Salaam.  Mtoto wa Mwanamuziki wa dansi Nguza Viking ‘Babu  Seya’ Michael Nguza amesema anamshukuru Mungu baada ya Rais John Magufuli kutangaza familia yao ipo huru kuanzia leo Jumamosi.  Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo, leo Jumamosi, Desemba 2017 akiwa mjini Dodoma wakati wa akihutubia  maadhimisho miaka 56 ya sherehe za Uhuru wa Tanganyika. Michael Nguza ambaye hivi sasa anajiita Nabii Michael baada ya kutoka jela  amesema : “Namshukuru Mungu, Mungu ni mwaminifu. Siwezi kuongea mengi kwa sasa, nitatoa taarifa baadaye. “Tunatarajia kufanya kikao cha familia ili kujadili suala hili na baadaye tutaulezea umma baada ya majadiliano haya familia naomba kuweni wavumilivu,” amesema Nabii Michael.

Kufuatia kusamehewa kwa wafungwa, Chadema wampongeza rais Magufuli

Dar es Salaam.  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimempongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ahadi zilizotolewa na mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa ikiwemo ya kuwaachia huru wanamuziki Nguza Viking na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’. Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na chama hicho imeeleza kuwa katika ahadi zake Lowassa aliahidi iwapo Chadema ingeshinda uchaguzi angewaachia wanamuziki hao. Vilevile chama hicho  kimetoa wito kwa  Serikali kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa sheria kuondoa nia ya kuwashtaki masheikh wa Zanzibar na mahabusu na washtakiwa wa makosa ya mtandao. Ombi hilo pia limewagusa mahabusu wa makosa ya kisiasa, ikiwemo kesi za uchochezi zinazohusisha kumkosoa Rais, chama  na serikali yake.

Breaking News: Papii Kocha na Babu Seya wapata msamaha wa Rais

Rais Dkt. John Magufuli ametoa msahama kwa wasanii Papii Kocha na baba yake Nguza Viking a.k.a Babu Seya waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela. Rais Magufuli amesema hayo leo mjini Dodoma wakati wa sherehe za miaka 66 ya Uhuru. Pia Rais Magufuli ametoa msamaha kwa watu 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa. Nguza Viking na Papii Kocha walikuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto wadogo wa shule ya msingi.

Wabunge wa Chadema waachiwa kwa Dhamana

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro imetupilia mbali hati ya kiapo cha kupinga dhamana ya wabunge Suzan Kiwanga(Mlimba), Peter Lijualikali (Kilombero) na washtakiwa wengine 37 waliofikishwa mahakamani hapo kwa makosa nane. Mbele ya Hakimu, Ivan Msaki mahakama ilitupilia mbali kiapo hicho na kueleza kuwa washtakiwa wote dhamana yao iko wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja watakaosaini dhamana ya Sh 5 milioni na pia barua za dhamana lazima zisainiwe na wenyeviti wa vijiji ama maofisa watendaji. Katika kiapo kilichowasilishwa awali mahakamani hapo na upande wa mashtaka kupitia wanasheria wa Serikali, Sunday Hyera na Edga Bantulaki ulieleza sababu walizodai kuwa ni za msingi za kupinga dhamana na kwamba kuwepo nje kwa washtakiwa  kunaweza kuharibu upelelezi wa kesi hiyo. Kufuatia hoja hiyo upande wa utetezi unaowakilishwa na mawakili wanne wakiongozwa na wakili Peter Kibatala uliamua kuwasilisha hati ya kupinga kiapo hicho kwa madai kuwa  kil

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kuuawa kwa askari 14 DRC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha askari 14 wa Jeshi la JWTZ kuuawa walipokuwa katika operesheni ya kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Zitto Kabwe azungumzia hatima ya ACT- Wazalenddo

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amefunguka kuwa  ndani ya chama chake (ACT) kuna watu wengi wakiwemo wanachama wa kutosha  akimaanisha hajabaki mwenyewe. Zitto amefunguka hayo akimjibu mfuasi wake wa kwenye mtandao wa kijamii ambaye alitoa maoni yake kwa kumuuliza Mh. Kabwe haoni kama amebaki peke yake, ikiwa ni muda mfupi baada ya aliyekuwa Mgombea urais wa chama chake Anna Mghwira kujiunga na CCM huko Dodoma. Akimjibu mfuasi huyo Zitto amesema "Chama chetu ACT Wazalendo kina madiwani 42, kina wenyeviti wa mitaa, vitongoji na wajumbe wa Serikali za Vijiji/Mitaa 507, Viongozi kila mkoa na jimbo, wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu. Ni dhahiri tuna watu wengi na wanachama wengi wa kutosha" Hivi karibuni CCM ilijivunia wanachama wapya ambao waliwahi kuwa na nafasi ya uongozi ACT Wazalendo ambapo baadhi yao ni Prof Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba, Alberto Msando na jana  Anna Mghwira.

MHITIMU WA DARASA LA SABA ABAKWA,AUAWA KISHA KUTUPWA MAKABURINI

Mwili wa mtoto Lucia Thomas ambaye amefanyiwa ukatili ukiwa ndani ya Jeneza ukiagwa na kusafirishwa kwenda  w ilayani Bunda m koani Mara kwa ajili ya mazishi. Baadhi ya majirani,ndugu,jamaa na marafiki wakiwa nje kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu. Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkoani, Salvatory Edward akisisitiza kufungwa kwa vituo bubu vya kufundishia wanafunzi kwenye mtaa ambao anauongoza.  Mchungaji wa Kanisa la Heri wenye moyo safi , Samwel Samson akihubiri na kutoa neno la faraja kwa familia. Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye hali ya masikitiko na maombolezo.  Picha na Joel Maduka,Geita *** Mtoto Lucia Thomas mwenye umri wa miaka 12 amekutwa akiwa ameuawa na mwili wake kutupwa eneo la makaburi mtaa wa mkoani mjini Geita. Mwenyekiti wa mtaa wa Mkoani, Salvatory Edward amedai pamoja na kunyongwa hadi kufa, mwili wa mtoto huyo aliyehitimu darasa la saba mwaka huu katika Shule ya Msingi Kiandege wilayani Bunda pia ulikuwa na dalili za kubakwa kabla

MAGAZETI YA LEO 9/12/2017