Skip to main content

Mtoto wa Babu Seya, Michael Nguza afunguka haya baada ya familia yao kuwa huru

Dar es Salaam. Mtoto wa Mwanamuziki wa dansi Nguza Viking ‘Babu  Seya’ Michael Nguza amesema anamshukuru Mungu baada ya Rais John Magufuli kutangaza familia yao ipo huru kuanzia leo Jumamosi.

 Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo, leo Jumamosi, Desemba 2017 akiwa mjini Dodoma wakati wa akihutubia  maadhimisho miaka 56 ya sherehe za Uhuru wa Tanganyika.

Michael Nguza ambaye hivi sasa anajiita Nabii Michael baada ya kutoka jela  amesema : “Namshukuru Mungu, Mungu ni mwaminifu. Siwezi kuongea mengi kwa sasa, nitatoa taarifa baadaye.

“Tunatarajia kufanya kikao cha familia ili kujadili suala hili na baadaye tutaulezea umma baada ya majadiliano haya familia naomba kuweni wavumilivu,” amesema Nabii Michael.

Comments