Skip to main content

Kufuatia kusamehewa kwa wafungwa, Chadema wampongeza rais Magufuli

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimempongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ahadi zilizotolewa na mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa ikiwemo ya kuwaachia huru wanamuziki Nguza Viking na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na chama hicho imeeleza kuwa katika ahadi zake Lowassa aliahidi iwapo Chadema ingeshinda uchaguzi angewaachia wanamuziki hao.

Vilevile chama hicho  kimetoa wito kwa  Serikali kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa sheria kuondoa nia ya kuwashtaki masheikh wa Zanzibar na mahabusu na washtakiwa wa makosa ya mtandao.

Ombi hilo pia limewagusa mahabusu wa makosa ya kisiasa, ikiwemo kesi za uchochezi zinazohusisha kumkosoa Rais, chama  na serikali yake.

Comments