Skip to main content

Tundu Lissu afunguka

Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu ambaye anaendelea na matibabu nchini Kenya jijini Nairobi amefunguka na kusema kuwa wanaendelea kupigana na watashinda vita hiyo.

Lissu amesema hayo baada ya kukutana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jusa Ladhu alipomtembelea jijini Nairobi katika hospitali anayopatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.

"Leo nina furaha sana kwa kupata fursa ya kumtembelea sahib na ndugu yangu, Tundu Lissu, Nairobi Hospital anakoendelea kupata matibabu baada ya kupigwa risasi zipatazo 16 mwilini Septemba 7, mwaka huu. Amenambia nikufikishieni ujumbe huu: "We keep up the fight and we shall win" alindika Jussa kwenye mtandao wake wa twitter

Mbali na hilo Jussa amedai kuwa afya ya Tundu Lissu kwa sasa inaendelea vizuri sana

"Anaendelea vizuri sana. Mimi leo nilivyomuona sikuamini jinsi anavyopata nafuu. Kwa hakika ni Qudra ya Mwenyezi Mungu. Tuendelee kumuombea dua apone haraka arudi kwenye shughuli zake"

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...