Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2017

Kikwete Amvaa Kigwangallah

Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amemvaa Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Khamis Kigwangala na kumwambia anaweza kuwa sehemu ya wachochezi kwa anachokifanya. Ridhiwani Kikwete amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya  Mhe. Kigwangalla kuonyesha kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma katika kuwafanyia usaili baadhi ya wataalamu waliojitokeza kwenye usaili  wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao umefanyika mapema leo Agosti 30, 2017. "Unaweza dhani unauliza swali kumbe nawe unakuwa sehemu ya wachochezi! Mhe. Waziri unaweza kuwa hujui kusoma lakini picha inatoa jibu sahihi",  aliandika Ridhiwani. Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma leo Agosti 30, 2017 ilifanya usaili kwa ajili ya nafasi za kazi katika Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambapo takribani watu 30,000 walijitokeza huku ikiwa watu 400 pekee ndiyo wanaotakiwa.

RC Makonda kasitisha bomoabomoa ya Nyumba Dar Es Salaam

Serikali imesema kutokana na utapeli na uuzaji holela wa viwanja eneo la Toangoma wilayani Temeke, hakuna atakayebomolewa nyumba eneo hilo. Kauli hiyo inayotokana na agizo la Rais John Magufuli imetolewa leo Agosti 30, wakati tayari nyumba zipatazo 300 zimewekwa alama ya X kuashiria kuwa zinapaswa kubomolewa. Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Masaki, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema, "Rais Magufuli aliniambia hamkumchagua ili awabomolee nyumba zenu bali awaboreshee makazi na kuwaletea maendeleo." Serikali pia, imeagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua dhidi ya watu wote waliohusika na uuzwaji wa maeneo na kufanya udanganyifu. Wananchi kwa upande wao wametakiwa kujiepusha na ujenzi holela na kununua viwanja kwa njia isiyo halali ili kuepuka usumbufu. Uongozi wa Wilaya ya Temeke juzi Agosti 28 uliitisha kikao na wananchi wanaodaiwa kujenga katika eneo linalodaiwa kuwa la Serikali lililotengwa kwa ajili ya kuendeleza ukanda wa kijani linalojuli

Bodi ya Mikopo Yaongeza Muda wa Uombaji Mikopo hadi 11/9/2017

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa wanafunzi kuwasilisha maombi ya mikopo. Hatua hiyo imeelezwa inalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi walioshindwa kufuata masharti kuyakamilisha. Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema muda huo umeongezwa hadi Septemba 11 badala ya Septemba 4. “Tumesogeza mbele kwa siku saba zaidi ili walioshindwa kufuata vigezo wakati wa kujaza fomu wafanye hivyo,” amesema. Amesema hadi kufikia jana Agosti 29, wanafunzi waliojitokeza walikuwa 49,282 lakini ni 15,473 waliokamilisha maombi kwa njia ya mtandao. mwananchi

Shahidi Asimulia Alivyomsikia Tundu Lissu Akiikashifu Serikali

Shahidi  wa tano wa Jamhuri katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), amedai mahakamani kwamba alipomsikia mtuhumiwa akitamka Rais Dk. John Magufuli ni rais uchwara na ni rais dikteta, alisogea pembeni, hakuendelea kusikiliza. Shahidi huyo, Timos Emekea (44), alidai hayo jana wakati akiongozwa kutoa ushahidi wake na Wakili wa Serikali, Paul Kadushi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Alidai aliona baadhi ya askari wanasogea kutokana na maneno ya Lissu na akahisi kuna kitu kinaweza kutoka, hivyo akajiondokea na safari zake. Emekea ambaye ni mkazi wa Goba, alidai siku  hiyo ya tukio ya Juni 28, 2016 alikuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akimdhamini mfanyakazi wake saa tano asubuhi. Alidai akiwa mahakamani hapo, aliona umati wa wananchi, waandishi wa habari na Lissu ambaye huwa anamuona kwenye TV alizungumza maneno ambayo hakupendezwa nayo. Wakili Peter Kibat

Msafara wa Mkuu wa Wilaya Washambuliwa Kwa Mapanga Na Mishale

Msafara  wa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Godfrey Mheluka, umeshambuliwa na wananchi katika Kijiji cha Kashanda, Kata ya Nyakahanga alipokwenda kufuatilia mgogoro wa wafugaji na wakulima. Katika mashambulizi hayo, Diwani wa Kata ya Nyakahanga, Charles Bechumila (CCM), amejeruhiwa vibaya kwa mishale na kukimbizwa katika Hospitali Teule ya Nyakahanga kutibiwa na alifanyiwa upasuaji huku hali yake ikielezwa kuwa ni mbaya. Ilidaiwa kuwa mkuu huyo wa wilaya alikwenda kijijini hapo kutoa tamko kuhusu mgogoro wa wakulima na wafugaji akiwa na msafara wa magari mawili. Katika gari lake alikuwa amepanda na Katibu Tawala wa Wilaya (DAS), Innocent Msena na Ofisa Uhamiaji mmoja na askari polisi wawili. Gari la pili katika msafara huo lilikuwa na Diwani Bechumila, maofisa tarafa wawili na waandishi wa habari wawili wa Redio Karagwe. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Ulomi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa askari waliokuwa wameambata

Tundu Lissu Amlima Barua Jaji Mkuu.....Adai Wanasheria Waliosusia Mgomo Alioutangaza Hawana Mshikamano

Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kimemwandikia barua Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma, kumwelezea sababu za mgomo wao na jinsi wanasheria wanavyonyanyaswa na kuuawa. Mgomo huo wa siku mbili unatokana na shambulio la mabomu katika Ofisi ya Mawakili ya IMMMA. Barua hiyo ya TLS iliyotiwa saini na Rais Tundu Lissu, imesema mgomo wao wa siku mbili haumaanishi kupingana na Serikali au kuwaadhibu wateja ila kuhamasisha umma kuhusu mazingira ya hatari waliyopo wanasheria nchini. Lissu alisema tukio hilo halikufanyika kwa bahati mbaya na matukio kama hayo ya kuwasumbua wanasheria wasifanye kazi zao ipasavyo, imekuwa sehemu ya maisha yao. “Kwa mfano, Aprili 7, mwaka jana ofisi za Mwanasheria Said Omar Shaaban ambaye kwa sasa ni Rais wa Chama Wanasheria wa Zanzibar (ZLS), zilipigwa bomu na kuharibiwa, lakini hadi leo hakuna ripoti ya uchunguzi wa polisi. “Wanasheria pia wamefungwa  kizuizini na wengine kukamatwa wakiwa mahakamani wakitekeleza majukumu yao ya

Hospitali ya Kairuki Yatoa Ufafanuzi Tuhuma za Mgonjwa Kuachwa na Vifaa vya Upasuaji Tumboni na Ukeni

Tume Yakupambana na Picha na Video za Ngono Yaundwa

Serikali ya Uganda imeunda tume maalum pamoja na kuitengea bajeti ya pesa itakayotoka kila mwaka kwa ajili ya kudhibiti usambazaji wa picha, video na vitu vingine vinavyochochea ngono. Imeelezwa kuwa maamuzi hayo yamefikiwa ili kuokoa nguvu kazi ya taifa ambayo imeathiriwa kwa kiasi kikubwa kutokana na watu wengi nchini humo kuendekeza masuala ya ngono. Kwa mujibu wa Waziri wa Maadili wa Uganda, Simon Lokodo, tume hiyo itakayokuwa na wajumbe tisa na watalaam wengine kati ya 30 hadi 40 itatengewa bajeti ya Shilingi Bilioni 2 kila mwaka. Bw. Lokodo amefafanua kwamba, tume hiyo itakuwa na vifaa vya kisasa kuingilia watu wanaohusika na kusambaza, kupakua, na kuangalia picha na video za ngono kisha kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria. Amedai kuwa vitendo hivyo vinaliangamiza taifa hilo kwa kuchochea ongezeko la mimba za utotoni, matumizi ya dawa za kulevya, ushoga na ubakaji.

Majambazi wateka basi, wapora madiwani

MAJAMBAZI sita wameteka basi la Kampuni ya Safi na likitokea Kijiji cha Mamba wilayani Chunya kwenda jijini Mbeya na kisha kuwapora abiria jana. Miongoni mwa waliotekwa ni pamoja na baadhi ya madiwani waliokuwa wakielekea mjini Chunya kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani Maalumu kwa ajili ya kupitia na kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika jana. Akizungumzia tukio hilo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Ramadhani Shumbi aliyekuwa mmoja wa waathirika wa uvamizi huo, alisema tukio hilo lilitokea saa moja kasorobo asubuhi katika eneo la Loge. Shumbi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mamba, alisema walipofika eneo hilo lililo na msitu mkubwa, walikuta kuna gogo kubwa lililolazwa na kufunga barabara na kisha walijitokeza watu sita mmoja akiwa amebeba bunduki na wengine mapanga na fimbo. Alisema watu hao walipiga risasi tatu hewani na kuanza kupiga vioo vya basi wakiwaamuru abiria washuke, lakini iliwachukua

Baraza la usalama la UN laionya Korea Kaskazini

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo cha Korea Kaskazini cha kurusha kombora kupitia anga ya Japan, huku nchi hiyo ikithibitisha kutekeleza. Taarifa iliyoandikwa na Marekani, haikutishia kuiwekea vikwazo vipya Korea kaskazini. Lakini Baraza la Usalama limeitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio zaidi na kusitisha mpango wake wa nuklia. Wanachama 15 wa Baraza hilo la Usalama wameitaka Korea Kaskazini kuchukua hatua za haraka kupunguza hali ya wasiwasi uliyopo. Majeshi ya Korea Kusini na Marekani yamekuwa yakifanya mazoezi ya pamoja karibu na mpaka wa Korea Kaskazini, jambo ambalo Pyongyang inasema ni mazoezi yenye kulenga uvamizi wa kijeshi.

MAGAZETI YA LEO 30/8/2017

Mzozo wa Korea Kaskazini na Marekani kwa muktasari

Mzozo unaohusisha Korea Kaskazini ni mzozo ambao unaweza hata kusababisha vita vya vinyuklia, vita ambavyo huenda pengine haviwezi vikawa na mshindi. Lakini ni mzozo wenye mambo mengi tata. Hebu tuchanganue kiasi. Ni kwa nini Korea Kaskazini inataka silaha za nyuklia? Rais ya Korea iligawanyika na kuwa mataifa mawili baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na kukawa na Korea Kaskazini na Kusini. Korea Kaskazini iliegemea siasa za Kikomunisti na iliongozwa na serikali ya kiimla, uongozi sawa na wa Stalin katika Muungano wa Usovieti. Marafiki wake wakuu ni Urusi na Uchina. Nchi hiyo ilijitenga pakubwa na nchi nyingine, isipokuwa nchi kadha marafiki wake. Viongozi wa nchi hiyo wanasema silaha za nyuklia ndiyo njia pekee ya kujikinga dhidi ya maadui kutoka nje ambao wanataka kuliangamiza taifa hilo. Wamekaribia kiasi gani ? Majaribio yake ya karibuni zaidi ya makombora yanaachilia kwamba nchi hiyo inakaribia sana kuwa na makombora ya kuruka kutoka bara moja hadi jingine yanayofah

Walimu Watiwa mbaroni kwa kufanya mapenzi na wanafunzi

Walimu wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha tatu shuleni hapo. Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, January Lugangika amesema waalimu wa wanafunzi hao wamekikuka maadili ya ualimu na kwamba watachukuliwa hatua zaidi huku akiongeza kuwa tabia hizo zinaleta kichefu chefu kwa jamii. Aidha mwenyekiti huyo amedai kuwa ushahidi wa tukio hilo umethibitishwa na Daktari ambaye aliwafanyia vipimo na kuthibitisha ni kweli kitendo hicho kilifanyika Kwa upande wa Afisa elimu wa sekondari Wilaya ya Lushoto Kassim Singato amesema endapo kutakuwa na masomo ya ziada ni lazima yafahamike muda yanapoisha ili wazazi waweze kufuatilia mwenendo wa watoto wao. "Inabidi wazazi muwafatilie watoto wenu kwa kila hatua, mjue wanafanya nini shuleni na kama mzazi humfat

Rais Magufuli Kuwa Mgeni Rasmi Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa

Rais John Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa 33 wa kawaida wa Jumuia ya Tawala za Mitaa (Alat). Mwenyekiti wa Alat, Gulamhafeez Mukadam amesema, awali mkutano huo ulipangwa kufanyika Septemba 19 hadi 22 lakini kutokana na baadhi ya wanachama kutokusanya fedha kwa wakati, umesogezwa na sasa utafanyika Oktoba 2 hadi 5 mkoani Mbeya. Amesema kutokana na mamlaka za Serikali za mitaa kuwa wanachama wa Alat na Rais ndiye mwenye dhamana na Serikali za Mitaa, hivyo atakuwa mgeni rasmi katika mkutano huo. Amesema pamoja na mambo mengin e, mkutano huo ni fursa ya kuwakutanisha viongozi wakuu wa Serikali Kuu na za mitaa kwa ajili ya kutoa maelekezo na miongozo ya kisera kwa watekelezaji ambao ni mamlaka ya serikali za mitaa nchini. Mukadam amesema kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ardhi kwenye mamlaka ya Serikali za Mitaa ni chachu ya maendeleo, halmashauri zitenge ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vidogovidogo na vikubwa". Amsema," Tutatumia mkutano huu kujik

Ndondi: Cheka, Miyeyusho wafungiwa na TPBC

Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) limewafungia na kuwapiga faini ya Tsh. 200,000/ mabondia Cosmas Cheka na Francis Miyeyusho wakidaiwa kufanya vurugu baada ya kushindwa katika mapambano yao. Shirikisho hilo limechukua hatua hizo kutokana na fujo zilizotokea usiku wa kuamkia jumapili katika michezo iliyofanyika ukumbi wa Vijana Social hall Kinondoni Dar es salaam. Kutokana na kitendo hicho kamisheni imewaonya Bondia wote watakao jihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani wakati wa michezo mahali popote kuwa watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kulipa faini. Hata hivyo TPBC imewaomba radhi kwa fujo zilizotokea na kuwaahidi kutotokea tena mahali popote. Adhabu za mabondio hao zinatarajia kuanza kutekelezwa Septemba 5 mwaka huu.

Shule 29 zafungiwa Manispaa ya Ubungo

Shule 29 za msingi na awali katika Manispaa ya Ubungo zimefungiwa kwa kukosa usajili baada ya ukaguzi unaoendelea wa kukagua shule zote katika Manispaa hiyo . Afisa Habari wa Manispaa ya Ubungo Bornwell Kapinga amesema zoezi hilo lilianza juzi na kuwa baada ya kubaini shule hizo hazina usajili walizifungia hadi hapo zitakapofuata taratibu za kusajili. "Ukaguzi huu ulifanywa kwa kushirikiana na Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Ubungo, Chausiku Masegenya ambapo waliwaagiza wamiliki shule hizo  kufuata taratibu za usajili na endapo hamtafanya hivyo wahamisheni wanafunzi na muwapeleka katika shule nyingine. Natoa wito kwa wamiliki wote wa shule mfuate taratibu pindi mnapotaka kuwekeza kwenye elimu kwani ubora wa elimu unaanzia katika usajili", alisema Bornwell. Pamoja na hayo, Bornwell amesema lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuboresha elimu katika manispaa hiyo lakini pia kudhibiti  utitiri wa shule lukuki ambazo zimekuwa zikifunguliwa kiholela katika manispaa hiyo ambazo pia

Kenya: Jaji wa mahakama ya juu augua kesi ya upinzani kupinga matokeo ya urais ikiendelea

Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu nchini Kenya ameugua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais ikiendelea kusikizwa. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu David Maraga, ambaye ndiye kiongozi wa mahakama hiyo, Jaji Mohammed Ibrahim, mmoja wa majaji saba ambao wamekuwa wakisikiliza kesi hiyo iliyowasilishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga alianza kuugua kabla ya vikao vya leo kuanza na alihudumiwa na madaktari. Kuugua kwake kuliwaacha majaji sita wakisikiliza hoja za pande mbalimbali katika kesi hiyo. Majaji hao wengine ni Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, Prof Jackton Boma Ojwang, Bi Njoki Ndung'u, Isaac Lenaola na Dkt Smokin Wanjala. Bw Odinga amepinga hatua ya Tume ya Uchaguzi (IEBC) kumtangaza Rais Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 8 Agosti. Majaji hao wanatarajiwa kutoa uamuzi wao kufikia Ijumaa tarehe 1 Septemba. Kwa mujibu wa matokeo ya IEBC, Rais Kenyatta alipata kura 8,203,290 huku naye Raila Odinga akipata kura 6,762,224.

Walichojadili RC Makonda na Kamanda mpya wa Polisi Dsm

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amefanya Mazungumzo na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Lazaro Mambosasa aliekuja kuripoti kwa Mkuu wa Mkoa baada ya kuteuliwa  hivi karibuni na IGP Simon Sirro.  Katika Mazungumzo hayo wamejadili hali ya UsalamaJijini Dar es Salaam na namna ya kuendeleza yale ambayo yaliachwa na IGP Simon Sirro wakati akiwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Mbunge wa Tunduma akamatwa na polisi

Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka amekamatwa na polisi akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mjini Vwawa. Mwakajoka amekamatwa leo Agosti 29 baada ya kufika mahakamani hapo kufuatilia kesi inayomkabili mbunge mwenzake wa Mbozi, Pascal Haonga. Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbozi, James Mbasha amesema mbunge huyo amekamatwa lakini hajui kosa linalomkabili. Mbasha amesema alipata taarifa leo asubuhi kwamba mbunge huyo anatafutwa na polisi. Katika kesi mahakamani hapo, Haonga na wenzake wawili Wilfred Mwalusanya na Mashaka Mwampashi wanakabiliwa na mashtaka mawili, kufanya vurugu na kuwazuia askari kufanya kazi yao kinyume cha sheria. Mwendesha mashitaka wa polisi, Samwel Saro anadai jana Agosti 28 saa saba mchana, washtakiwa walimzuia askari kutimiza majukumu yake ya kumkamata Mwampashi aliyedaiwa kwamba si mjumbe halali katika uchaguzi wa mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlowo. Washtakiwa pia wanadaiwa kumfanyia vurugu msimamizi wa uchaguzi

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande

Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi Hatua  ya kwanza Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki. Hatua ya pili Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke. Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa. Hatua ya tatu Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi. Njia ya pili Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo. Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla sabuni haijawa ngumu mwaga sabuni ndani ya kasha la mbao lilotangulizwa