Skip to main content

Majambazi wateka basi, wapora madiwani

MAJAMBAZI sita wameteka basi la Kampuni ya Safi na likitokea Kijiji cha Mamba wilayani Chunya kwenda jijini Mbeya na kisha kuwapora abiria jana.

Miongoni mwa waliotekwa ni pamoja na baadhi ya madiwani waliokuwa wakielekea mjini Chunya kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani Maalumu kwa ajili ya kupitia na kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika jana.

Akizungumzia tukio hilo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Ramadhani Shumbi aliyekuwa mmoja wa waathirika wa uvamizi huo, alisema tukio hilo lilitokea saa moja kasorobo asubuhi katika eneo la Loge.

Shumbi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mamba, alisema walipofika eneo hilo lililo na msitu mkubwa, walikuta kuna gogo kubwa lililolazwa na kufunga barabara na kisha walijitokeza watu sita mmoja akiwa amebeba bunduki na wengine mapanga na fimbo.

Alisema watu hao walipiga risasi tatu hewani na kuanza kupiga vioo vya basi wakiwaamuru abiria washuke, lakini iliwachukua abiria takribani dakika 10 wakigoma kushuka kabla ya baadhi walioonekana kutishika zaidi kuanza kushuka kwa kuruka kupitia madirishani.

Alisema baadaye iliwalazimu abiria wote kushuka na ndipo jambazi wakaanza kuwasachi na kunyang’anya fedha taslimu na simu za mikononi huku walioonekana kubisha, wakipigwa.

“Baada ya kushuka tulilazwa chini na kuanza kukaguliwa ambapo walichukua fedha na simu na mimi mwenyewe ni mhathrika wa simu na fedha kidogo nilizokuwa nazo. Ushauri wangu ni kuwa mabasi kama haya yaanze safari saa moja asubuhi badala ya saa kumi na moja ama kumi na mbili,” alieleza diwani huyo.

Comments

Popular posts

Alikiba akata kiu ya mashabiki wake kwa staili hii

                  Msanii Alikiba Msanii  Alikiba ambaye yupo kimya kwa muda mrefu ameamua kukata kiu ya mashabiki wake na kumaliza hasira zao kwa kushusha ngoma tatu mfululizo pindi atakaporejea Tanzania kutokea nchini Marekani alipokwenda kwa ajili ya kufanya show. Siku mbili zilizopita Alikiba kupitia mitandao yake ya kijamii alianza kuweka post ambayo ilionyesha ni ishara ya ujio wake mpya baada ya kuweka 'post' iliyokuwa na jina la 'Kipusa' na kuaindikia maneno kuwa "Wananiita Kipusa' baada ya siku moja aliweka nyingine iliyokuwa inasema 'they call me a heartbreaker" hali ambayo ilianza kuwachanganya mashabiki wake wengine wakidhani kuwa ni mistari kutoka kwenye wimbo huo.  Lakini siku moja mbele aliweka post nyingine inayosema 'Pasua Kichwa' hali ambayo ilizidi kuongeza maswali mengi kwa mashabiki wake, lakini mdogo wake na Alikiba anayefahamika kwa jina la Zabibu ameweka wazi kaka yake Alikiba ataachia kazi tat...

Baraza la usalama la UN laionya Korea Kaskazini

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo cha Korea Kaskazini cha kurusha kombora kupitia anga ya Japan, huku nchi hiyo ikithibitisha kutekeleza. Taarifa iliyoandikwa na Marekani, haikutishia kuiwekea vikwazo vipya Korea kaskazini. Lakini Baraza la Usalama limeitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio zaidi na kusitisha mpango wake wa nuklia. Wanachama 15 wa Baraza hilo la Usalama wameitaka Korea Kaskazini kuchukua hatua za haraka kupunguza hali ya wasiwasi uliyopo. Majeshi ya Korea Kusini na Marekani yamekuwa yakifanya mazoezi ya pamoja karibu na mpaka wa Korea Kaskazini, jambo ambalo Pyongyang inasema ni mazoezi yenye kulenga uvamizi wa kijeshi.