Skip to main content

Ndondi: Cheka, Miyeyusho wafungiwa na TPBC

Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) limewafungia na kuwapiga faini ya Tsh. 200,000/ mabondia Cosmas Cheka na Francis Miyeyusho wakidaiwa kufanya vurugu baada ya kushindwa katika mapambano yao.

Shirikisho hilo limechukua hatua hizo kutokana na fujo zilizotokea usiku wa kuamkia jumapili katika michezo iliyofanyika ukumbi wa Vijana Social hall Kinondoni Dar es salaam.

Kutokana na kitendo hicho kamisheni imewaonya Bondia wote watakao jihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani wakati wa michezo mahali popote kuwa watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kulipa faini.

Hata hivyo TPBC imewaomba radhi kwa fujo zilizotokea na kuwaahidi kutotokea tena mahali popote.
Adhabu za mabondio hao zinatarajia kuanza kutekelezwa Septemba 5 mwaka huu.


Comments