Skip to main content

Walimu Watiwa mbaroni kwa kufanya mapenzi na wanafunzi

Walimu wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha tatu shuleni hapo.

Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, January Lugangika amesema waalimu wa wanafunzi hao wamekikuka maadili ya ualimu na kwamba watachukuliwa hatua zaidi huku akiongeza kuwa tabia hizo zinaleta kichefu chefu kwa jamii.

Aidha mwenyekiti huyo amedai kuwa ushahidi wa tukio hilo umethibitishwa na Daktari ambaye aliwafanyia vipimo na kuthibitisha ni kweli kitendo hicho kilifanyika

Kwa upande wa Afisa elimu wa sekondari Wilaya ya Lushoto Kassim Singato amesema endapo kutakuwa na masomo ya ziada ni lazima yafahamike muda yanapoisha ili wazazi waweze kufuatilia mwenendo wa watoto wao.

"Inabidi wazazi muwafatilie watoto wenu kwa kila hatua, mjue wanafanya nini shuleni na kama mzazi humfatilii anaweza kufanya mambo usiyoyajua na badala yake ukashtukia ana mimba ya miezi hata sita," alisema Singato.

Watuhumiwa wa tukio hilo ni mwalimu Fredriki Shebila na Saddat Mohamed.

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...