Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu ambaye anaendelea na matibabu nchini Kenya jijini Nairobi amefunguka na kusema kuwa wanaendelea kupigana na watashinda vita hiyo. Lissu amesema hayo baada ya kukutana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jusa Ladhu alipomtembelea jijini Nairobi katika hospitali anayopatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma. "Leo nina furaha sana kwa kupata fursa ya kumtembelea sahib na ndugu yangu, Tundu Lissu, Nairobi Hospital anakoendelea kupata matibabu baada ya kupigwa risasi zipatazo 16 mwilini Septemba 7, mwaka huu. Amenambia nikufikishieni ujumbe huu: "We keep up the fight and we shall win" alindika Jussa kwenye mtandao wake wa twitter Mbali na hilo Jussa amedai kuwa afya ya Tundu Lissu kwa sasa inaendelea vizuri sana "Anaendelea vizuri sana. Mimi leo nilivyomuona sikuamini jinsi anavyopata nafuu. Kwa hakika ni Qudra ya Mwenyezi Mun...