Skip to main content

Maoni ya Zitto kuhusu Baraza jipya la Mawaziri

                   
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT -Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ametoa maoni yake juu ya Baraza jipya la Mawaziri lililofanyiwa mabadiliko hii leo, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Kwenye ukurasa wake wa Facebook Zitto Kabwe ameandika ujumbe akiwapongeza Mawaziri hao walioteuliwa ambao wengi wao ni vijana, huku akiwataka kuchapa kazi kwa bidii.

"Uteuzi wa vijana kushika nafasi za juu ni hatua nzuri, naona vijana wengi wamepewa majukumu makubwa, ninawaombea watekeleze majukumu kwa weledi mkubwa", ameandika Zitto Kabwe.

Leo Rais Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuongeza wizara mpya mbili, baada ya kuzivunja baadhi ya wizara ambazo zilikuwa na vitengo vingi.


Comments