Skip to main content

Yanga yaambulia sare Songea

MZIMBABWE Donald Dombo Ngoma leo ameinusuru timu yake, Yanga SC kupoteza mechi mbele ya Maji Maji baada ya kuifungia bao la kusawazisha kipindi cha pili, timu hizo zikitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Maji Maji mjini Songea katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Ngoma alifunga bao la kusawazisha dakika ya 79 kwa kichwa akimalizia krosi ya Mzambia, Obrey Chirwa kumtungua kipa wa zamani wa Simba, Andrew Ntalla.

Hiyo ilifuatia Maji Maji kutangulia kwa bao la Peter Mapunda dakika ya 54 akimalizia pasi ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Jerson John Tegete kumtungua kipa Mcameroon Youthe Rostand.

Kipindi cha kwanza wenyeji Maji Maji walitawala mchezo na kufika mara nyingi kwenye eneo la hatari la Yanga, lakini hawakuweza tu kufunga kutokana na utulivu wa safu ya ulinzi ya mabingwa hao watetezi chini ya beki mkongwe, Kevin Yondan.

Sifa zaidi zimuendee kipa Mcameroon, Rostand aliyeokoa michomo mingi ya hatari likiwemo shuti la mpira wa adhabu la Mapunda kutoka upande wa kushoto ambalo alilipangua pembezoni mwa lango juu na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Yanga walicheza kwa kasi nzuri ya kushambulia kwa dakika 10 tu za mwanzo, baada ya hapo wakalizimika kucheza kwa kuwadhibiti zaidi wenyeji walioanza kutawala mchezo.

Lakini dakika tano kuelekea mapumziko, Yanga nao wakaanza kuwasukuma langoni mwao Maji Maji ambao nao walisimama imara kuondoa hatari zote upande wao.

Kipindi cha pili, Maji Maji walikianza vizuri baada ya mabadiliko yaliyofanywa na kocha Habib Kondo akiwaingiza wakongwe, kiungo wa zamani wa Simba, Abdulhalim Humud na mshambuliaji Tegete kuchukua nafasi za Yakubu Kibiga na Danny Mrwanda.

Maji Maji ikaenda kuuteka kabisa mchezo katika safu ya kiungo na kuanza kuwashambulia Yanga mfululizo kabla ya kupata bao la kuongoza.  Baada ya kufungwa, Yanga wakaamua kutoka kwenda kushambulia hadi kufanikiwa kupata bao la kusawazisha.  

Na baada ya Yanga kusawazisha timu hizo zilianza kushabuliana kwa zamu, huku zikicheza kwa tahadhari zaidi. Winga wa Yanga, Emmanuel Martin aliumia na kukimbizwa hospitali dakika ya 85 baada ya kugongana na mchezaji wa Maji Maji, Marcel Kaheza.

Kwa matokeo hayo, Yanga inafikisha pointi tano baada ya kucheza mechi tatu, ikitoa sare mbili na kushinda moja, lakini Maji Maji inafikisha pointi mbili baada ya kufungwa mechi moja na sare mbili.

Kikosi cha Maji Maji kilikuwa; Andrew Ntala, Juma Salamba, Mpoki Mwakinyuke, Kennedy Kipepe, Tumba Sued, Hassan Hamisi, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Yakubu Kibiga/Abdulhalim Humud dk46, Danny Mrwanda/Jerry Tegete dk46, Marcel Kaheza na Peter Mapunda.

Yanga SC; Youthe Rostand, Juma Abdul/Hassan Kessy dk65, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kevin Yondan, Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa, Raphael Daudi, Donald Ngoma, Ibrahim Hajib na Geoffrey Mwashiuya/Eammnuel Martin dk75/Said Juma ‘Makapu’ dk85.

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...