Skip to main content

Yafahamu Madhara Ya Kunywa Pombe Kipindi Cha Ujauzito

Kipindi cha ujauzito kwa mama ni kipindi muhimu sana ambacho kwa wakati huu mama hatakiwi atumie kitu chochote cha kujitibu bila ushauri wa daktari kwani kinaweza kudhuru mtoto lakini pia kipindi cha ujauzito ni kipindi ambacho mama hatakiwi kunywa kileo chochote kile unachokifahamu.

Sio bia, sio spirit, wala mvinyo au wine. wanawake wengi wa siku hizi hubeba mimba bila kufahamu kwamba wana mimba na huja kugundua baada ya mwezi mmoja au miwili baada ya kumshindilia mtoto pombe za kutosha.tabia hii ina madhara makubwa sana kwa mama na mtoto kama ifuatavyo...

1. Mtoto kua na umbo la ajabu; mtoto huweza kuzaliwa na kichwa kidogo, uso kama bapa na macho madogo sana. dalili hizi huweza kuanza kuonekana katika umri wa miaka 2 na mara nyingi mtoto hua tofauti na wenzake.

2. Kuchelewa kukua; pombe huingilia mfumo wa ukuaji na kumchelewesha mtoto kufanya baadhi ya mambo kama kutambaa, kutembea, kuongea na kadhalika. ukimuangalia mtoto mwenye umri kama huo huo ataonekana mkubwa kuliko huyu anayetumia pombe.

3. Kushindwa kujifunza; mara nyingi watoto hawa hua wabovu sana darasani na kushindwa kuelewa vitu kama watoto wengine..mata nyingi mzazi huishia kulalamika na kumshangaa mtoto na kumuona mzembe bila kujua chanzo ni yeye...

4. Kuchelewa kula kwa mtoto; kawaida mtoto anatakiwa anywe maziwa tu kwa muda wa miezi sita, tena maziwa ya mama baada ya hapo aanze kula chakula. mtoto aliyepata madhara ya pombe hushindwa kunyonya na kuchukua muda mrefu sana kuanza kula.

5. Matatizo ya viungo; siku hizi kuna picha zinatumwa sana mitandaoni zikionyesha mtoto kazaliwa bila mikono, miguu au kaunganikana kichwa na pacha mwenzake. hizo sio bahati mbaya kama watu wanavyodhani ila hayo ni madhara ya vitu ikiwemo pombe.

6. Kuharibika kwa ujauzito; pombe inaweza kuingilia mfumo wa homoni za mwanamke au kufungua mlango wa uzazi na kusababisha kuharibika kwa mimba, mimba huweza kuharibika ghafla au taratibu kulingana na aina ya pombe.

7. Kuzaa kabla ya muda; kwenye mimba kubwa pombe inaweza kusababisha kuanza kwa uchungu kabla ya muda na kumzaa mtoto ambaye hajakomaa maarufu kama kabichi.

Mwisho; hakuna kipindi ambacho ni salama kunywa pombe kipindi cha ujauzito, kama hauhitaji mtoto kwa sasa tumia vizuizi vya mimba lakini kama unakunywa pombe na kufanya ngono bila kinga utajikuta una mimba ambayo imeshaathirika na pombe tayari na ukipata mimba acha pombe kabisa.

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...