Skip to main content

Tundu Lissu Aitisha Mgomo wa Mawikili Nchi Nzima

Wadi Ahmedabad.

India inaonekana kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nguruwe baada ya watu 1,094 kuthibitishwa kufariki kutokana na ugonjwa huo katika kipindi cha miezi minane iliyopita, taarifa rasmi ya serikali imesema.
Katika wiki tatu zilizopita, idadi ya vifo imekuwa juu sana, ambapo watu 342 wamefariki.
Jumla ya visa 22,186 vya maambukizi ya ugonjwa huo vimeripotiwa nchini humo.
Idadi ya watu waliofariki mwaka huu ni mara nne zaidi ya idadi iliyoripotiwa katika kipindi sawa na hicho mwaka 2016 ambapo visa vya ugonjwa huo vilikuwa vimeshuka sana.
Jimbo la Maharashtra magharibi mwa nchi hiyo ndilo lililoathirika zaidi ambapo waliofarikini ni 437 kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya.
Jimbo hilo linafuatwa na jimbo jirani la Gujarat lililoshuhudia vifo 297.
India ilikabiliwa na mlipuko mbaya wa homa hiyo miaka miwili iliyopita ambapo zaidi ya watu 1,900 walifariki.
Lakini visa vilishuka mwaka 2016 ambapo ni watu 265 waliofariki, lakini mwaka huu visa vimeongezeka tena.
Mlipuko mbaya zaidi wa homa hiyo nchini humo ulitokea 2009-2010, ambapo watu 50,000 waliambukizwa na wengine 2,700 kufariki kote nchini humo.
Dkt Sanjay Gururaj, mkurugenzi wa kimatibabu katika hospitali ya Shanthi, ambayo ni hospitali ya kibinafsi, amesema si lazima kwa hospitali za kibinafsi kupiga ripoti kuhusu visa vya maambukizi ya homa hiyo kwa serikali.
"Takwimu za serikali kwa hivyo zinaweza kuwa ni kionjo tu," amesema.

Homa ya nguruwe ni nini?
  • Ni ugonjwa wa kupumua unaosababishwa na virusi ya influenza aina A, vinavyofahamika kama H1N1
  • Chanzo chake ni kwenye nguruwe, lakini sasa huambukiza binadamu na huenezwa kwa kupiga chafya au kukohoa.
  • Dalili za ugonjwa huo zinakaribiana na za homa ya msimu - homa kali, kukohoa, maumivu kooni, maumivu mwilini na mzizimo.
  • Wanaoathirika zaidi huwa wajawazito, watoto wa chini ya miaka mitano, wazee wa zaidi ya miaka 65 na wale wenye matatizo mengine ya kiafya.
  • Virusi hiyo vilitambuliwa mara ya kwanza nchini mexico mwaka 2009 na vikaenea upesi maeneo mengine duniani

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...