Skip to main content

Tottenham v Chelsea nani mbabe leo

Uwanja wa Wembley sio uwanja rafiki kwa Tottenham na ni kati ya viwanja mashabiki wa Tottenham hawavipendi lakini leo wanataka kuvunja mwiko na kuondoa laana katika uwanja huo, ikumbukwe huu ni mchezo wa kwanza wa Epl kupigwa katika dimba la Wembley.

Tottenham wanakutana na Chelsea ambao kwa misimu miwili mfululizo wamekuwa wakiwafunga katika michezo muhimu, msimu wa mwaka juzi Chelsea walizima ndoto za ubingwa za Tot na wakafanya tena msimu uliopita, Chelsea wamefungwa mara 2 tu na Tot katika mechi 17 zilizopita.

Tottenham wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu za kufungwa na Chelsea katika michezo muhimu lakini leo Tottenham wanaingia na matumaini kwani kikosi cha Chelsea kinaonekana hakijakaa vizuri.

Chelsea wanaingia katika mchezo huu huku Cesc Fabregas,Garry Cahil,Pedro,Eden Hazard na Diego Costa wakiwa hawapo kwa matatizo mbali mbali ikiwemo adhabu na majeraha na hii inaweza kuwapa nafasi kubwa Tot kuifunga Chelsea.

Tottenham mshambuliaji wao Heung Mi Son anaweza kurejea leo baada ya majeraha yake kuanza kupona huku Danny Rose akiwa kwenye hati hati kukosa mchezo huu kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu.

Chelsea wanaweza kuzidi kupoteana hii leo na kipigo kutoka kwa Tottenham kinaweza kuanza kuchafua hali ya hewa katika klabu ya Chelsea ambapo tayari wachambuzi mbalimbali wameanza kutoa nafasi kwa Antonio Conte kuwa kocha wa kwanza kutimuliwa EPL msimu huu.

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Tanzania yakiri ununuzi wa Bombadier uko matatani

Tindu Lissu Serikali ya Tanzania imekiri kudaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd kama ambavyo kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tindu Lissu alivyo tangaza hivi karibuni. Kiongozi huyo amesema kuwa kumekuwa na athari za Serikali kuvunja mikataba ya wawekezaji wa nje kwani wanasheria wanaoishauri serikali wamekuwa hawatekelezi wajibu wao inawezekana ni kwa sababu ya kuogopa kutumbuliwa. Lissu ambaye ni mwanasheria Mkuu wa Chadema alidai Ijumaa kuwa utekelezaji wa ununuzi wa ndege ya tatu kutoka kampuni ya Bombadier ya nchini Canada umezuiliwa nchini Canada na kampuni hiyo ya ujenzi kwa kuwa inaidai serikali Dola 38.7 milioni za Marekani (Sh 87 bilioni). Vyanzo vya habari vinasema kuwa kampuni hiyo ilipewa kibali cha kukamata mali za Tanzania na Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro katika nchi za Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ubelgiji, Uganda na Canada. Lakini kwa upande wake serikali imesisitiza kuwa licha ya deni hilo, ndege hiyo ita...