Skip to main content

Tetesi za usajili, Mourinho kumfuatilia Ivan Perisic


Tottenham wamefikia makubaliano ya kimsingi ya kumsajili Davinson Sanchez, 21, kutoka Ajax kwa pauni milioni 28 na milioni 14 zaidi kama marupurupu.
Manchester City wapo tayari kuwapa West Brom pauni milioni 22 ili kumsajili nahodha wao Jonny Evans, 29, baada ya dau la pauni milioni 18 kukataliwa, na watampa mara mbili ya mshahara wa pauni 75,000 kwa wiki anaolipwa sasa.
Dau la Chelsea la pauni milioni 62 kumtaka beki wa Juventus Alex Sandro, limekataliwa.
Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Costa alifunga mabao 20 katika mechi 35 alizochezea Chelsea na kuwasaidia kushinda ligi msimu uliopita
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Robert Fernandez amesema itakuwa “vigumu” kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, kwa sababu hana kipengele cha uhamisho kwenye mkataba wake.
Barcelona “watapigana” mpaka siku ya mwisho ya usajili ili kumsajili Philippe Coutinho kutoka Liverpool. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, amesema hatorudi Stamford Bridge na anataka kujiunga na Atletico Madrid.
Beki wa Tottenham Kevin Wimmer, 24, anazungumza na Stoke City kuhusu uhamisho wake wa pauni milioni 15. (Telegraph)
Stoke City pia wanataka kumsajili Kevin Wimmer kutoka Spurs. (Stoke Sentinel)
Beki wa Arsenal Gabriel, 26, anakaribia kujiunga na Valencia kwa pauni milioni 10. (Evening Standard)
Paris Saint-Germain bado wanataka kumsajili kiungo mkabaji wa Monaco, Fabinho, 23.
Kiungo wa PSG Blaise Matuidi, 30, amekamilisha vipimo vya afya Juventus, lakini timu hizo mbili bado hazijakubaliana jinsi ada ya uhamisho itakavyolipwa, huku meneja wa PSG Unai Emery akisema hakutaka kumuuza mchezaji huyo.

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...