Skip to main content

Serikali Yamjibu Tundu Lissu Sakata la Ndege Kushikilia Canada kisa Madeni


Serikali kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa imejibu hoja zilizotolewa na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kuhusu kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania aina ya Bombadier Q-400 Dash 8 nchini Canada.

Zamaradi Kawawa amekiri kuwa ni kweli ununuzi wa ndege hizo umeingiliwa na mgogoro na kukiri kuwa ndege hiyo Q-400 Dash 8 inashikiliwa nchini Canada kwa madai ya kuwa ndege hiyo imeshikiliwa kwa mgogoro wa kutengeneza na wanasiasa wa Tanzania wasioitakia mema nchi ya Tanzania.

"Ununuzi wa ndege ya 3 ya Bombadier umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania, Wanasiasa waliotengeneza mgogoro huo wanahujumu maendeleo ya nchi na usalama wa raia" alisema Zamaradi Kawawa

Aidha Zamaradi Kawawa amesema kuwa ndege ya tatu ambayo ilikuwa inatarajiwa kuingia nchini mwezi Julai amedai kuwa itaingia muda si mrefu na kuwataka Watanzania waiamini serikali ya Tanzania iliyopo chini ya Rais John Pombe Magufuli

"Ndege ya 3 ya Bombadier ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini Serikali yao ila serikali imesikitishwa na ushiriki wa wanasiasa na baadhi ya watu kuhujumu maendeleo ya nchi, Watanzania tuwe wazalendo kulinda, kutetea na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo ya Nchi, tuunge mkono jitihada za Rais Magufuli  katika kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya chama, kabila au dini" alisisitiza Zamaradi Kawawa

Mbali na hilo Kawawa amesema kuwa serikali imeanza kuchukua hatua kadhaa kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hizo

"Kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hatua za Kidiplomasia na sheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili" alisema Zamaradi Kawawa

Hapo Jana Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia Na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema ndege hiyo imeshindwa kuwasili nchini kufuatia kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya Serikali ya Tanzania nakupelekea kukamatwa kwa Ndege hiyo mali ya Tanazania. 

Comments

Popular posts

Grace Mugabe ashindwa kuhudhuria mkutano wa SADC Afrika Kusini

Mke wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, amakosa kuhudhudia mkutano wa kanda nchini Afrika Kusini. Grace Mugabe, 52, anataka kupewa kinga ya kidiplomasia baada ya kulaumiwa kumshambulia mwanamitindo nchini Afrika Kusini wiki iliyopita. Alikuwa ahudhurie mkutano na wake wa marais kwenye mkutano huo wa SADC Mamlaka zinasema kuwa anasalia nchini Afrika Kusini wakati ombi lake la kutaka apewe kinga ya kidiplomasia likiendelea kushughulikiwa. Polisi wanataka kumhoji kuhusu madai hayo. Polisi wameweka ulinzi mkali kwenye mipaka ya taifa hilo kuhakikisha kwamba Bi. Mugabe hatatoroka. Mwamitindo Gabriella Engels 20, alimshtumu Bi Mugabe kwa kumpiga baada ya kumpata akiwa na watoto wake wawili wavulana ndani ya chumba kimoja cha hoteli huko Sandton, mtaa mmoja wa kifahari kaskazini mwa mji wa Johannesburg Bi Engels aliambia BBC kwamba alishambuliwa na bi Mugabe aliyeamini kwamba alikuwa akijua kule aliko mwanawe Bellarmine. ''Tuliendelea kumwambia hatujui aliko...hatujamuona usiku wote...