Skip to main content

Serikali Yakanusha Kumpa Siku 7 Tundu Lissu Kuomba Msamaha

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kwamba imempa siku 7 Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu kuomba radhi kwa kupotosha umma

Kwenye ukurasa wa twitter wa msemaji wa serikali ametoa taarifa akisema kuwa taarifa hizo si za kweli, kwani hata mtu aliyetumika kuandika hiyo taarifa yupo msibani.

"Umma unaarifiwa kuwa baada ya tamko la jana Serikali haijatoa tamko lolote tena.Uzushi unaosambazwa mitandaoni  Jumapili hii  ni wa kupuuzwa, taarifa inayosambazwa ni ya uongo kwa kuwa hata Dkt. Abbas anayetajwa kusaini bado yuko likizo ya kufiwa. Hatua kali zitachukuliwa", aliandika twitter ya Msemaji wa serikali.
Hapo awali kulikuwa na taarifa iliyosambaa ikionyesha imetoka serikalini, ikimtaka Mh. Tundu Lissu kuomba radhi huku ikimpa siku 7 tu za kufanya hivyo.

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...