Skip to main content

Polisi watoa taarifa Kuhusu tukio la mlipuko ofisi za mawakili



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

28/08/2017
               TUKIO LA MLIPUKO KWENYE OFISI ZA MAWAKILI WA IMMA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 26/8/2017 lilitoa taarifa ya awali ya tukio la mlipuko uliotokea katika ofisi za mawakili wa IMMA zilizopo katika eneo la Upanga jijini Dar Es Salaam.

Hivyo Jeshi la Polisi linapenda kuufahamisha umma kuwa  uchunguzi wa awali uliofanyika umebaini kwamba usiku wa kuamkia tarehe 26/8/2017 majira kati ya saa 7:00-8:00 watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi kamili, walifika katika ofisi za mawakili wa kampuni ya IMMA (IMMA ADVOCATES) wakiwa na magari mawili wakijifanya ni askari na kuwarubuni kisha kuwachukua walinzi wa jengo hilo na kuondoka nao kwenye moja ya gari walilokwenda nalo,ambapo baadaye walinzi hao walikutwa maeneo ya Kawe wakiwa hawajitambui.

Aidha, kundi lililobaki liliingia ndani ya Ofisi hizo na kuweka milipuko iliyotengenezwa kienyeji ambayo baada ya watu hao kuondoka ililipuka na kusababisha uhalibifu wa mali na jengo la ofisi hiyo pamoja na majengo ya jirani.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm linapenda kuwahakikishia wananchi kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini watu hao waliofanya tukio hilo pamoja na kujua dhamira yao ili wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.

Aidha tunapenda ifahamike kuwa wajibu wa Jeshi la Polisi ni kulinda maisha ya watu na mali zao  hivyo kamwe haliwezi kutumika kuhujumu maisha ya watu na mali za wananchi.

Tunaomba waathirika wa tukio hili na wananchi kwa ujumla kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na upelelezi wa tukio. Vilevile, tunatoa rai kwa wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia katika upelelezi waziwasilishe kwa Jeshi la Polisi ili zifanyiwe kazi. 

B.M. KITALIKA- SACP
KAIMU KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...