Skip to main content

Mbunge amtaka Magufuli kumuiga Kenyatta na kuruhusu maandamano

Rais John Pombe MagufuliRais John Pombe Magufuli
Mbunge wa Arusha mjini nchini Tanzania kupitia Chadema, Godbless Lema amemtaka rais John Pombe Magufuli kumuiga mwenzake wa Kenyatta Uhuru Kenyatta kupitia kuwaruhusu wapinzani wake wa kisiasa kufanya siasa zao bila vikwazo, kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania.
Akihutubia mkutano wa umma katika wadi ya Murieti, Lema alimsifu rais Kenyatta na kusema ameoonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwaruhusu wapinzani wanaomtuhumu kwamba alihusika na udanganyifu katika uchaguzi mkuu uliokamilika hivi majuzi kufanya maandamano mbali na kuwapatia maafisa wa usalama kuwalinda
Kulingana na gazeti hilo ,Rais Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa akitetea kiti chake aliibuka mshindi katika uchaguzi huo kwa kupata asilimia 54 ya kura huku mpinzani wake Raila Odinga akijipatia asilimia 44.
Kulingana na Lema maandamano ya upinzani pamoja na mikutano ya uma itaisaidia serikali kwa sababu chama tawala kitaelewa maswala yanayowakabili raia na kuyafanyia kazi huku upinzani ukitekeleza haki yao ya kidemokrasia kupitia kushirikiana na umma mbali na kutatua maswala muhimu yanayowakabili raia.
''Demokrasi ni swala tata, mara nyengine linaweza kuathiri uchumi. Wawekezaji wengi huchunguza kiwango cha demokrasia katika taifa kabla ya kuwekeza. Iwapo tutaendelea na mkondo huu basi utatukwaza katika siku za usoni'', alisema

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...