Skip to main content

Mazishi ya pamoja yafanywa Sierra Leone kwa mamia ya maiti

Maiti 150 za watu walioangamia kwenye maporomoko ya matope nchini Sierra Leone zimezikwa jana mjini Freetown. Imebainika kuwa miongoni mwa walioangamia ni watoto 105.

Erdrutsch in Sierra Leone Sicherheitskräfte Schutzmasken (picture-alliance/AP/M. Kamara)
Mazishi ya pamoja ya mamia ya maiti zilizotokana na maporomoko ya matope siku tatu zilizopita yamefanywa jana katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown. Aidha kuna hofu kuwa mvua zaidi inayotarajiwa kunyesha huenda ikalemaza juhudi za uokozi wakati ambapo watu 600 bado hawajulikani waliko. Wakati huo huo, serikali imelaumiwa kwa mpango mbovu wa ujenzi katika mji huo.
Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, maiti 150 za watu walioangamia kwenye maporomoko hayo ya matope yaliyotokea siku ya Jumatatu baada ya mvua kubwa iliyonyesha, tayari zimezikwa leo kwenye kaburi la pamoja mjini Freetown.
Jamaa aliyezidiwa na majonzi nje ya hospitali ya Connaught
Jamaa aliyezidiwa na majonzi nje ya hospitali ya Connaught
Haya yanajiri huku serikali ikikabiliwa na ukosoaji mkali wa kutofanya lolote dhidi ya ukataji miti wa kiholela na mpango mbovu wa mjini ambapo baadhi ya wakazi wamejenga chini ya milima na kuondoa mawe au miamba ambayo huzuia matope wakati wa mvua.
Idhaa ya Kiingereza ya DW imezungumza na msemaji wa shirika la Msalaba mwekundu nchini humo Mathew Cochrina na haya ndiyo amesema. "Tunaamini kuwa hadi sasa familia 1,100 zimeathirika, wengi wao hawana makao baada ya nyumba zao kuharibiwa, ni janga kubwa la kibinadamu, na shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu zinaendelea. La muhimu zaidi ni kwamba manusura wanahitaji ushauri nasaha." 
Imebainika kuwa miongoni mwa walioangamia ni watoto 105. Watu wengine wamesema wamepoteza jamaa zao wote pamoja na mali. Watu 600 bado hawajulikani waliko. Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa takriban watu 3000 wamepoteza makao kufuatia mkasa huo na huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Shughuli za uokozi zikiendelea
Shughuli za uokozi zikiendelea
Raia pamoja na wataalamu wanaibua maswali ya ni kwa nini serikali ya rais Ernest Bai Koroma haijafanya jambo kudhibiti ujenzi wa nyumba kinyume cha sheria katika mji wa Freetown ambao tayari unakumbwa na msongamano wa wakaazi.
Katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Connaught, miili kadhaa imetapakaa. Maafisa wa Koroma wamesema miili ambayo haijatambuliwa itazikwa katika siku chache zijazo. Aidha Sierra Leone ambayo maelfu ya raia wake waliangamia miaka michache iliyopita kutokana na mripuko wa Ebola, imeomba misaada kutoka kwa jamii ya kimataifa, huku ikiweka mipango maalum ya kuzuia miripuko ya magonjwa kama kipindupindu.
Huku shughuli za uokozi zikiendelea, tabiri za hali ya anga za juma lijalo zinaonesha kuwa mvua itanyesha na hivyo huenda maporomoko zaidi ya matope yakatokea.
Malkia Elizabeth II wa Uingereza ametuma risala za rambirambi kwa Rais Koroma huku akielezea kusikitishwa na mkasa huo.

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Tanzania yakiri ununuzi wa Bombadier uko matatani

Tindu Lissu Serikali ya Tanzania imekiri kudaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd kama ambavyo kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tindu Lissu alivyo tangaza hivi karibuni. Kiongozi huyo amesema kuwa kumekuwa na athari za Serikali kuvunja mikataba ya wawekezaji wa nje kwani wanasheria wanaoishauri serikali wamekuwa hawatekelezi wajibu wao inawezekana ni kwa sababu ya kuogopa kutumbuliwa. Lissu ambaye ni mwanasheria Mkuu wa Chadema alidai Ijumaa kuwa utekelezaji wa ununuzi wa ndege ya tatu kutoka kampuni ya Bombadier ya nchini Canada umezuiliwa nchini Canada na kampuni hiyo ya ujenzi kwa kuwa inaidai serikali Dola 38.7 milioni za Marekani (Sh 87 bilioni). Vyanzo vya habari vinasema kuwa kampuni hiyo ilipewa kibali cha kukamata mali za Tanzania na Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro katika nchi za Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ubelgiji, Uganda na Canada. Lakini kwa upande wake serikali imesisitiza kuwa licha ya deni hilo, ndege hiyo ita...