Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameomba msaada wa boti kwa jeshi la China kwa ajili ya kukabiliana na wahalifu wa madawa ya kulevya.
Makonda ameomba msaada huo alipotembelewa na viongozi wa jeshi la China ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Makonda amewaomba kumsaidia kuwapatia vifaa vya kutumiwa na askari wa doria katika Bahari ya Hindi ili waweze kukabiliana na wahalifu wenye kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya.
Pia Makonda ameeleza kuwa ujio wa viongozi hao umejadili pia masuala mengi ya ushirikiano baina ya watu wa nchi hizi mbili na kuhakikisha usalama wa wao na ushirikiano mwingine wa nyanja mbalimbali.
Naye Mkuu wa Kikosi cha Maji cha China (Navy), Shen Hao, amepongeza juhudi za mkuu huyo wa mkoa hasa za kuhakikisha anapambana na watu wanaoingiza madawa ya kulevya wakipitishia pembezoni mwa Bahari ya Hindi na akasema ushirikiano wa nchi yake na nchi ya Tanzania utaendelea kuwa imara.
Comments