Skip to main content

KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI KWA AJILI YA UHAKIKI WA TUZO MBALIMBALI KWA WALE WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA SHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)
 
TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI KWA AJILI YA UHAKIKI WA TUZO MBALIMBALI KWA WALE WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA SHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limepokea maombi ya wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi na Vyuo kuhusu kuongezwa kwa muda wa kuhakiki Tuzo za Stashahada kwa wale wanaopenda kujiendeleza katika ngazi ya Shahada katika Vyuo vya Elimu ya Juu.

Hivyo Baraza linapenda kuwafahamisha wadau na wahitimu wa Stashahada wanaotaka kujiendeleza katika ngazi ya Shahada kuwa muda wa kufanya maombi ya uhakiki wa Tuzo zao umeongezwa hadiTarehe 23 Agosti, 2017.

Hivyo kwa wale ambao hawakufanikiwa kumaliza maombi ya uhakiki na wale ambao hawajaomba na wana nia ya kufanya hivyo, sasa wataweza kufanya uhakiki.

Baraza linapenda kutoa rai kwa waombaji kufanya uhakiki wa Tuzo zao mapema ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza katika dakika za mwisho wa muda wa uhakiki.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 18 Agosti, 2017

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Tanzania yakiri ununuzi wa Bombadier uko matatani

Tindu Lissu Serikali ya Tanzania imekiri kudaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd kama ambavyo kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tindu Lissu alivyo tangaza hivi karibuni. Kiongozi huyo amesema kuwa kumekuwa na athari za Serikali kuvunja mikataba ya wawekezaji wa nje kwani wanasheria wanaoishauri serikali wamekuwa hawatekelezi wajibu wao inawezekana ni kwa sababu ya kuogopa kutumbuliwa. Lissu ambaye ni mwanasheria Mkuu wa Chadema alidai Ijumaa kuwa utekelezaji wa ununuzi wa ndege ya tatu kutoka kampuni ya Bombadier ya nchini Canada umezuiliwa nchini Canada na kampuni hiyo ya ujenzi kwa kuwa inaidai serikali Dola 38.7 milioni za Marekani (Sh 87 bilioni). Vyanzo vya habari vinasema kuwa kampuni hiyo ilipewa kibali cha kukamata mali za Tanzania na Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro katika nchi za Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ubelgiji, Uganda na Canada. Lakini kwa upande wake serikali imesisitiza kuwa licha ya deni hilo, ndege hiyo ita...