Skip to main content

Kiongozi Kenya aamua kumuiga Rais Magufuli.

Gavana mteule wa jimbo la Nairobi nchini Kenya Mike Sonko, ameingia kitendo cha Rais Magufuli alichofanya baada ya kuingia madarakani cha kuingia mtaani na kufanya usafi, huku akiweka kampeni maalum ya usafi.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Mike Sonko ameweka picha na kuandika kuwa serikali yake itasimima suala hilo ili kuweka mji safi, ili kutunza mazingira na kujiepusha na magonjwa ya kumbukiza.

“Ni muhimu kwetu kujua na kuweka mazingira safi  kwani muhimu kwa maisha yetu, na serikali yangu itawezesha kila kinachohitajika ili kufanya usafi, ili kuonyesha dhamira yetu tumetoa  mapipa ya kutunzia takataka 20, mikokoteni 10, koleo 10, reki 10, viatu, mipira ya mikono  na vitu vingine kwa kila kata hapa Nairobi,  kwa kazi za kawaida:”, aliandika Sonko.

Sonko aliendelea kuandika “Tukitaka kuondokana na kipindu pindu a magonjwa mengine mabaya, tunahitaji kuweka mazingira yetu safi, nahimiza kuacha kutupa taka hovyo, tutumie hivi vifaa ipasavyo na kuhakikisha tunasafisha makazi yetu”, aliandika Sonko.

Mike Sonko aliendelea kusema kuwa wakifanikisha hilo wataweza kuepukana pia na mafuriko, na kuwataka watu wa Nairobi kuwa mawakala wa usafi.


Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...