Skip to main content

Hospitali ya Kairuki Yashitakiwa Kwa Kufanya Opareshen na Kisha Kusahau Vitu Tumboni

Mkazi  wa jijini Dar es Salaam, Khairat Omary, ameishtaki Hospitali ya Kairuki na kudai fidia ya Sh milioni 155 kwa kumsababishia matatizo katika mfuko wa uzazi yaliyofanya aondolewe kizazi.

Khairat kupitia Kampuni ya Uwakili ya Jonas amefungua kesi ya madai namba 184 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na imepangwa kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Katika madai hayo, mdai anadai alikuwa akihudhuria kliniki wakati wa ujauzito katika hospitali hiyo na Desemba 15 mwaka jana alijifungua kwa upasuaji, akaruhusiwa Desemba 17 mwaka huo na kutakiwa kurudi tena Desemba 21.

Mdai akiwa nyumbani alianza kusikia maumivu ikiwamo kutapika, ilipofika Desemba 21 alirudi hospitali akaeleza maumivu anayopata kwa daktari ambaye alielekeza afanyiwe kipimo cha Ultra Sound.

Majibu yalipotoka daktari akampatia dawa za kutuliza maumivu na kumtaka apumzike hali itaendelea kuimarika.

“Akiwa nyumbani hali iliendelea kuwa mbaya, alisikia maumivu makali ya kichwa na alianza kubadilika rangi ambapo alikimbizwa hospitali ya jirani, walipompima wakaelekeza apelekwe Regency Hospital kwa matibabu zaidi.

“Regency walimfanyia vipimo na kubaini kuna tatizo katika mfuko wa uzazi na kumuhamishia Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia walimfanyia vipimo na kubaini wakati alipofanyiwa upasuaji kuna vitu vilibakia kama pamba ambavyo vimesababisha mfuko wa uzazi kuharibika,” ilisema sehemu ya hati hiyo ya madai.

Anadai ili kuokoa maisha yake alishauriwa kuondolewa kizazi, hata hivyo licha ya kuondolewa alibakia na tatizo la fĂ­stula lililosababishwa na pamba zilizoachwa wakati anajifungua.

Mdai anadai kutokana na uzembe huo wa kutokuwa makini wakati wa kumzalisha anaomba mahakama iamuru alipwe Sh milioni 20 gharama za matibabu, Sh milioni 25 fidia kwa kukosa kipato wakati anaumwa, Sh milioni 80 gharama za adhabu na Sh milioni 30 fidia.

Wadaiwa wanatakiwa kupeleka utete wao mahakamani na kesi hiyo itatajwa Agost 31, mwaka huu.

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Tanzania yakiri ununuzi wa Bombadier uko matatani

Tindu Lissu Serikali ya Tanzania imekiri kudaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd kama ambavyo kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tindu Lissu alivyo tangaza hivi karibuni. Kiongozi huyo amesema kuwa kumekuwa na athari za Serikali kuvunja mikataba ya wawekezaji wa nje kwani wanasheria wanaoishauri serikali wamekuwa hawatekelezi wajibu wao inawezekana ni kwa sababu ya kuogopa kutumbuliwa. Lissu ambaye ni mwanasheria Mkuu wa Chadema alidai Ijumaa kuwa utekelezaji wa ununuzi wa ndege ya tatu kutoka kampuni ya Bombadier ya nchini Canada umezuiliwa nchini Canada na kampuni hiyo ya ujenzi kwa kuwa inaidai serikali Dola 38.7 milioni za Marekani (Sh 87 bilioni). Vyanzo vya habari vinasema kuwa kampuni hiyo ilipewa kibali cha kukamata mali za Tanzania na Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro katika nchi za Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ubelgiji, Uganda na Canada. Lakini kwa upande wake serikali imesisitiza kuwa licha ya deni hilo, ndege hiyo ita...