Skip to main content

Godbless Lema: Tutaendelea Kumkoa Hadharani Rais Akikosea.....Akipatia Tutamsifia Hadharani Pia

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka na kusema kuwa wao kama viongozi watamsifu Rais pale anapofanya vizuri hadharani na kusema anapokosea lakini amedai hawawezi kumdhihaki Rais wala kusema mambo ya uongo dhidi yake.

Lema alisema hayo jana katika mkutano wake wa tisa jimboni kwake kwenye Kata ya Sekei Sanawari, Arusha Mjini na kusema anashangazwa na watu ambao wanasema Rais hatakiwi kusemwa hadharani.

"Sitaongea uongo hadharani na sipo hapa kumdhihaki Rais ila Rais akikosea nitamsema na sitamsema chumbani bali nitamsema hadharani, habari ya nchi inavyoendeshwa tunasema hadharani, Rais akikosea tutamsema hadharani na akipatia tutampongeza hadharani" alisema Godbless Lema

Aidha Mbunge Lema aliendelea kutoa lawama zake kwa viongozi mbalimbali wa dini akisema kuwa wamekuwa wakifumbia macho mbalimbali ambayo yanaendelea ndani ya nchi hivyo ameahidi kuwa akimaliza mikutano yake atakuja kufanya mikutano mingine kuhamasisha wanachi wasitoe sadaka kwa taasisi za dini kwa kuwa viongozi hao wamekuwa wakifumbia macho na kushindwa kusema juu ya ukiukwaji wa sheria ndani ya nchi na namna ambavyo Demokrasia imekupwa ikiminywa. 

Mbali na hilo Lema alisema anawashangaa watu wanaosema kuwa Mwanasheria wa CHADEMA Tundu Lissu siyo mzalendo kwa kuwa ameweza kusema kuwa kuna ndege ya Tanzania imeshikiliwa nchini Canada.

"Leo Lissu anakamatwa kwa sababu ya kusema ndege ya Tanzania imekamatwa kwa kuwa tunadaiwa Ulaya, Polisi wanamchukua Lissu na kwenda kumsachi kwake, mnatafuta ndege chumbani kwa mke wa Tundu Lissu, wanasema Lissu si mzalendo sasa nani mzalendo aliyesema tunadaiwa Ulaya au aliyetaka kuchukua fedha kinyemela akalipe deni Ulaya" alihoji Godbless Lema

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...