Skip to main content

Fid Q atamani kuwapatanisha Alikiba na Diamond

Mwanamuziki wa hip hop, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ amefunguka kwa kusema kuwa anataka kuwapatanisha mahasimu wawili kwenye muziki wa Bongo Fleva, Alikiba na Diamond Platnumz.

Fid ameweka wazi mpango wake huo ikiwa ni siku chache baada ya Diamond kutumia wimbo wake mpya ‘Fresh’ kufanya remix ambayo ndani yake alirusha makombora kwa Ali Kiba mara mbili.
Amesema kuwa mvutano wa kiushindani kwenye muziki huchangamsha muziki lakini unapofika mbali na kuhusisha maisha binafsi unaweza kuwa hatari na kuleta madhara, hivyo unapaswa kukemewa.
Diamond na AliKiba wamekuwa katika hali ya kutoelewana kwa muda mrefu ingawa mara kadhaa walisikika wakieleza kuwa hawana tofauti na kila mmoja kumuombea kura mwenzake kwenye tuzo za kimataifa.
Diamond alirusha makombora yake kwenye mshairi ya ‘Fresh Remix’ akirap lakini Ali Kiba alirudisha majibu yake kupitia mtandao wa Twitter.
Ugomvi huo pia uliomhusisha Ommy Dimpoz ambaye kupitia akaunti yake instagram aliweka picha akiwa na mama yake Diamond na kuandika maneno yasiyokuwa mazuri.

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...