Skip to main content

Atiwa mbaroni kwa kumpa mtoto kinyesi cha Mbuzi

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza, linamshikilia mkazi wa Mtaa wa Chakechake, Sospeter Rajabu (42), kwa kosa la kumpaka kinyesi  cha mbuzi kwenye majeraha yaliyotokana kuungua   moto  mtoto wake, Neema Sospeter (10) mwanafunzi wa darasa la  kwanza na kusababisha hali yake kuwa mbaya.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi jana, ilisema mtuhumiwa  alikamatwa juzi  saa 10:30 jioni  Mtaa wa Chakechake  wilayani  Nyamagana.

Alisema Sospeter anatuhumiwa  kumpaka mavi ya mbuzi  mtoto wake kwenye majeraha ya moto aliyoungua maeneo ya mapaja ya miguu yote miwili kwa muda wa wiki mbili na kusababisha  majeruhi kuwa na hali mbaya kiafya ambapo  wananchi walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo, askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi maeneo hayo na kufanikiwa kumkuta mtoto akiwa kwenye hali mbaya na  kushirikiana na wananchi kumkimbiza hospitali na  kumkamata baba wa mtoto.

“Huyu mtoto aliungua moto Agosti 4, mwaka huu saa 1:45 usiku  Mtaa wa Kitangiri wilayani Iilemela ambapo alikuwa akiishi na mama yake kwani wazazi wake walitengana kwa muda mrefu, inadaiwa alimwagikiwa na mafuta ya taa alipokuwa akiweka kwenye  kibatari na kuwasha  na njiti ya kibiriti na  moto kulilipuka kisha  kumuunguza.

“Baada ya mama yake  kukosa fedha za matibabu, aliamua kumpeleka  kwa baba yake Mtaa wa Chakechake alipokua akiishi na mke mwingine ili amsaidie mtoto apate matibabu, lakini baada ya mtoto kufikishwa kwa baba yake hakupelekwa hospitali na  badala yake alikuwa akipakwa mavi ya mbuzi na kusababisha  hali yake kuzidi kuwa mbaya,” alisema Kamanda Msangi.

Alisema polisi wapo kwenye upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa dhidi ya ukatili aliyokuwa akimtendea mwanae pindi uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani, majeruhi amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza  Sekou Toure akiendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Tanzania yakiri ununuzi wa Bombadier uko matatani

Tindu Lissu Serikali ya Tanzania imekiri kudaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd kama ambavyo kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tindu Lissu alivyo tangaza hivi karibuni. Kiongozi huyo amesema kuwa kumekuwa na athari za Serikali kuvunja mikataba ya wawekezaji wa nje kwani wanasheria wanaoishauri serikali wamekuwa hawatekelezi wajibu wao inawezekana ni kwa sababu ya kuogopa kutumbuliwa. Lissu ambaye ni mwanasheria Mkuu wa Chadema alidai Ijumaa kuwa utekelezaji wa ununuzi wa ndege ya tatu kutoka kampuni ya Bombadier ya nchini Canada umezuiliwa nchini Canada na kampuni hiyo ya ujenzi kwa kuwa inaidai serikali Dola 38.7 milioni za Marekani (Sh 87 bilioni). Vyanzo vya habari vinasema kuwa kampuni hiyo ilipewa kibali cha kukamata mali za Tanzania na Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro katika nchi za Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ubelgiji, Uganda na Canada. Lakini kwa upande wake serikali imesisitiza kuwa licha ya deni hilo, ndege hiyo ita...