Skip to main content

Alikiba akata kiu ya mashabiki wake kwa staili hii

Msanii Alikiba
Msanii Alikiba ambaye yupo kimya kwa muda mrefu ameamua kukata kiu ya mashabiki wake na kumaliza hasira zao kwa kushusha ngoma tatu mfululizo pindi atakaporejea Tanzania kutokea nchini Marekani alipokwenda kwa ajili ya kufanya show.

Siku mbili zilizopita Alikiba kupitia mitandao yake ya kijamii alianza kuweka post ambayo ilionyesha ni ishara ya ujio wake mpya baada ya kuweka 'post' iliyokuwa na jina la 'Kipusa' na kuaindikia maneno kuwa "Wananiita Kipusa' baada ya siku moja aliweka nyingine iliyokuwa inasema 'they call me a heartbreaker" hali ambayo ilianza kuwachanganya mashabiki wake wengine wakidhani kuwa ni mistari kutoka kwenye wimbo huo. 

Lakini siku moja mbele aliweka post nyingine inayosema 'Pasua Kichwa' hali ambayo ilizidi kuongeza maswali mengi kwa mashabiki wake, lakini mdogo wake na Alikiba anayefahamika kwa jina la Zabibu ameweka wazi kaka yake Alikiba ataachia kazi tatu kwa mpigo na kuwataka mashabiki wakae mkao wa kula pindi atakaporudi kutoka nchini Marekani ataachia kazi hizo. 

Alikiba siku ya Jumamosi ya tarehe 19 Agosti atakuwa akikiwasha nchini Marekani katika mji wa New York ambapo atakuwa na wasanii wengine kibao kutoka Afrika wakiwepo P Square, 2 Baba, Tiwa Savage pamoja na  Cassper Nyovest

Comments

Popular posts

Ugonjwa wasababisha Manji kutofika mahakamani

Mfanyabiashara nchini, Yusuf Manji ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili kutokana na kuwa mgonjwa. Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani hapo. Wakili wa serikali Estazia Wilson ameiambia Mahakama mbele ya Hakimu, Godfrey Mwambapa kuwa Manji hajafika Mahakamani hapo kwa vile ni mgonjwa ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu itakapotajwa tena. Manji na watuhumiwa wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na magari ya serikali. Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja, wote wamerudishwa rumande.

Mwanzo wa mwisho wa dunia utakuwa Jumatatu 21 Agosti?

Jua litapatwa na mwezi kikamilifu Amerika kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa Jumatatu tangu 1918 Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri san...